Naziru Ndimu, mkazi wa Mburahati, anatupa picha halisi ya mambo au shughuli mbalimbali zinazoendelea kila kukicha. Labda wengine tunapita tu mara moja moja sehemu husika, wengine tunapasikia tu, wengine tunaishi au ndugu zetu wanaishi huko, au wengine tunasoma habari juu ya vitongoji kama Mburahati; filamu hii itakusaidia kupata taswira inayokaribiana na hali halisi.
Huduma za kijamii zikoje? Huduma za afya? Wanafanyaje biashara? Je, wanajua haki zao?
Watu wa Mburahati wanakwambia ‘Dar ni Sisi’.
Bofya hapa kutazama filamu zaidi kama hizi.